Madereva (Leseni Daraja E)
Job Description:
Muhtasari wa Kazi
Mteja wetu anatafuta Madereva 30 wenye Leseni ya Daraja E wenye uzoefu wa kuendesha malori makubwa kwa ajili ya kusafirisha mizigo ndani ya Jiji la Dar es Salaam. Mwombaji anatakiwa kuwa mwangalifu, mwaminifu, na mwenye kufuata sheria za usalama barabarani pamoja na taratibu za kampuni.
Majukumu Makuu
- Kuendesha malori makubwa kwa usalama na ufanisi.
- Kusafirisha mizigo kulingana na ratiba na maeneo yaliyopangwa.
- Kukagua gari kabla na baada ya safari ili kuhakikisha liko katika hali nzuri.
- Kuripoti hitilafu, ajali au changamoto zozote za gari kwa wakati.
- Kuhakikisha mizigo imepangwa na kufungwa vizuri kabla ya safari.
- Kutunza kumbukumbu za safari na nyaraka za usafirishaji.
- Kuzingatia sheria za usalama barabarani na taratibu za kampuni.
- Kutunza usafi wa gari na kuhakikisha linafanyiwa matengenezo yanayohitajika.
- Kuwasiliana vizuri na wasimamizi pamoja na wateja pale inapohitajika.
- Kutekeleza majukumu mengine yanayohusiana na kazi utakayopangiwa.
Sifa na Vigezo
- Elimu ya Kidato cha Nne au zaidi.
- Awe na Leseni halali ya Udereva Daraja E.
- Uzoefu wa angalau miaka 3 wa kuendesha malori makubwa.
- Uelewa mzuri wa barabara za Dar es Salaam.
- Awe na historia nzuri ya uendeshaji wa magari.
- Awe na nidhamu, uaminifu na uwezo mzuri wa mawasiliano.
- Uwezo wa kufanya kazi kwa muda unaobadilika pale inapohitajika.
Mwisho wa Kutuma Maombi:
10 Agosti 2026